SURA YA TISA
Alidhania hawezi kufa hata alipowadhalimu na kuwatesa
wananchi wasio na hatia. Akaanza kupanga mazishi yake huku ajihisi
marehemu. Siku moja kamwita Amani na kumpa sururu, jembe na sepetu.
“nataka uchimbe hapa kaburi langu. Siku nitakapokufa nataka kuzikwa
hapa.” (uk 128) Ingawa Amani hakulitegemea, akawa hana budi ila
kukamilisha jukumu lake. Hivyo basi, akalichimba kaburi hilo kwa siku
tatu, likawa la fahari.
Mashaka kwake kukawa mashaka kweli, habebeki
mwana wa watu. “Abwajabwaja ovyoovyo kama Mzee matuko Weye. (uk 129)
Masomo keshaikatiza, nguo katupa na kuzura tupu mitaani. “Kumbe chema
hakidumu.” (uk 129) Madhubuti amejitolea kutumikia nchi yake kwa moyo
wake wote, tendo lililokuwa mkabala na alivyoamini baba mtu. “…alielewa
fika kwamba ingebidi aukate mkono uliokuwa ukimlisha tangu hapo hata
matokeo yake yakiwa nini.” (uk 130)
Mashaka akaleta rabsha na
kuwazidi wafanyikazi wengine. Bi Zuhura akamwita Amani na pamoja
wakamfungia Mashaka chumbani mwake. Kwa kuogofya yaliyokuwa yakiendelea,
Bi Zuhura akamsihi Amani kalale ukumbini. Nyakti za usiku, Amani
akaitwa na Bi Zuhura ili kaangalie ni nini kilichokuwa chini ya kitanda
chake mama mtu. Ni katika harakati hizi ndipo Bwana Mtemi akarejea na
kuwakuta wawili chumbani, wanatetemeka. “Ndani kukawa hakukaliki, nje
hakutokeki.” (uk 131) “Kumbe huyu mwanamke huniendea kinyume na
mfanyikazi jamani?” (uk 131) Akafungua sefu Mtemi, akatoa bunduki na
kumshambulia. Alipodiriki kwamba Amani kaaga dunia, akambeba kwenye buti
ya gari lake na kumtupa kando yam to Kiberenge, ambako aliokotwa na
Wasamaria wema na kupelekwa zahanati ya Nasaba Bora.
Kukawa siku nyingi zimepita Amani akiwa zahanatini. Alipofumbua macho na
kisha kuachwa huru, Imani wakaambatana na Majisifu kumpeleka kwake
Majisifu mwenyewe. Amani kufika nyumbani, akakubaliwa kukaa katika
“servants quarters” huku bado hawezi kuongea na kuwasiliana kwa
kuandika. Imani akamchunga kakake vizuri sana.
Amani akamfahamisha
Imani ya kuwa angependa kujistarehesha kwa kusoma vitabu. Imani
akamwazimia vitabu kutoka kwa Mwalimu Majisifu, ikiwemo kimoja kwa
anwani la “Kidagaa kimemwozea”. Kwa mshangao, kitabu chenye picha ndicho
kile chake, mswada aliyorudishiwa kwa kuwa hauwezi chapika. Majisifu
kajikuta taabani. “Lililomshangaza ni kwamba Yule aliyeitwa mwandishi na
kupachikwa picha yake katika jalada la nyuma, hakuwa ndiye mwandishi wa
kitabu hicho.” (uk 140) “…kilichokuwa chake kimekuwa cha mwingine.” (uk
141)
Amani akamwandikia Imani barua kumwelezea juu ya le aliyoyaona.
Majisifu akaipata barua ile na kuisoma. Hapo Imani akampata na
kumkabili vipasavyo. Majisifu akatoa zote siri alizokuwa amezibana,
“Kumbe umdhaniye ndiye siye?” Akamwandikia karatasi ndogo Amani kwa
Majisifu.
Betway Casino review for 2019 - Dr.MD
ReplyDeleteWe have the latest 충청북도 출장마사지 in 삼척 출장안마 the 남양주 출장샵 casino industry with all the latest in casino games, sports betting, casino 경상북도 출장마사지 promotions, free spins and more. Rating: 4.3 충청남도 출장안마 · 12 reviews