Sunday, February 7, 2016

KIDAGAA SURA YA NNE

                                     SURA YA NNE
“Siku tatu tangu Imani kende kwa nduguye nab ado hajaonekana.” (uk 49) Dora hakuweza kuvumilia kuwa linda wanawe. Akazidiwa hamaki na kumshambulia mumewe Bwana Majisifu ambaye kajibu kwa “kumfungulia cherehani ya matusi” (uk 52).
Hata hivyo, majibizano hayo yanakatizwa ghafla mlango unapobishwa na mpwa wake majisifu, Mashaka bintiye Mtemi Nasaba Bora. Majisifu na Dora wanavua nyuso za hasira na  kujibandika za bashasha, anagalau mgeni asijejua siri za jirani. Haisuru, wanaingia katka gumzo, ambapo Mwalimu Majisfu hachoki kumkosoa Mashaka.
Baada ya Dora na Mashaka kujiburudisha kwa chai, iliyosusiwa na Majisifu, kwani siku hizi kakosa tumbo la kuikarisha, sababu yenyewe keshazoea sharabu. Ndipo Mwalimu Majisifu anamwuliza mpwake kazi ambayo angependa kufanya baadaya ya masomo. “Napenda niwe mwandishi wa vitabu kama wewe amu”, (uk 47) akajibu Mashaka. Kwa kumalizia, Majisifu akaboronga lugha, “Kitanda usichokilalia hukijui kunguni wake” (uk 47).
Acha mashaka aulizie muda aliouchukua mwalimu Majisifu kukiandika kitabu chake cha “Kidagaa Kimemwozea”, jawabu likawa kaski mosi. “Aha, kurasa zote hizo?” akaendeleza mashaka. “Mwandishi bora lazima aandike haraka kabla mwazo hayajayeyuka kuwa upepo (uk 48).

Anapoondoka Mashaka, anampasa Mwalimu Majisifu barua inayomwalika Wangwani ili kutoa mihadhara kuhusu uandishi wake. Anamfahamisha Dora ambaye baada ya kuomba kuletewa “rinda na viatu toka Mkokotoni”, anaanza tena kushambuliana. “Kama utaweza, mbwa apige mswaki.” (uk 51). Anaghadhabika Mwalimu na kijibu kwa matusi. Hata hivyo tunajulishwa kwamba “nyoko nyoko” zilikuwa shibe za kawaida kwao.
Amani na Imani wanastakimu pamoja wakiwa na mwano wa kupagazwa, Uhuru. Hapa ndipo tunaelezwa vile wawili hawa walivyokutana na pia yale yaliyowatokea. Nyakti ni za usiku usiku, kuamkia sikukuu ya Uhuru. Wanasokomoko wengine, lao wanalo kushehekea kwa nyimbo na ngoma.
Mwinyihatibu mtembezi ambaye alikuwa mfanyikazi wa Mtemi alinunua shamba kule Baraka, alikoishi na familia yake akina Imani. Basi baba alipofariki, wakaja Askari na kudai kuwa sehemu ile ya ardhi lilikuwa na mwenyewe. Kupinga walipigwa na kuachwa hali mahututi. Oscar Kambona akatorokea na kudai kuja kulipiza kisasi. Baada ya mama mtu kuzikwa, wakaja Askari na kuchoma maskani ile, nusura Imani ateketee.

Marejesho hadi mwanzo wa safari hii ya waja hawa waili. Wanapokutana kando ya ziwa Mawewa, tunapomwona kijana mmoja, umri wa miaka isghirini hivi anaposoma hatujui nini.  Kisha anaitupa runda ile ya makaratasi baharini. Kumbe ilikuwa mswada ambao Amani kapeleka ili kuchapishwa,akarudishiwa kwa madai kwamba haikuwezekana  kuchapishwa. Kumbe Amani kachezewa karata, mswada wake ukaibiwa na kuchapishwa kwa jina la Majisifu Majimarefu. Hapa basi tunashangazwa kuona kwamba ni wale wanaofaa kuwa kiegezo kwa wnagenzi, ndio wanaobadilika kuwa paka kulinda kitoweo.
Wakati ambapo walikuwa wakipiga gumzo usiku kucha, mtoto Uhuru alilala fofofo. Ndugu hawa wa kupanga, wasiojuana, wazaziye Uhuru, mtoto wa kupagazwawakavuliana siri zao. Hata Amani aliyekuwa msiri kama kaburi hakuwa na jingine ila kudondoa alicho nacho rohoni.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Popular Posts

Unordered List

Pages

Categories

Labels

Download

Powered by Blogger.

Footer Widget 1

Text Widget

Blogger Tricks

Blogger Themes

Categories

Copyright © MWONGOZO NA UCHAMBUZI WA FASIHI ANDISH | Powered by Jkts Company 0706509638 |