SURA YA PILI
Eneo la Sokomoko ambako ni kwa matajiri. Kitambo kabla ya Uhuru, eneo
hili lilikuwa limetengewa Wazungu pekee. Wamiliki walipanda mimea
tofauti tofauti ikiwemo pareto, alizeti na kadhalika. Weusi
hawakuruhusiwa kuishi wala kulima mazao yoyote yaletayo fedha. Mweusi
angefuga tu mifugo ya kienyeji lakini njee ya Sokomoko.
Matajiri wa
Sokomoko waliyanyaka ardhi zile zilimilikiwa na wakoloni ambao walirudi
makwao. Miongoni mwa Wazungu hao, Major noon almaarufu Majujnuni ambaye
shamba lake lilinyakuliwa na Nasaba Bora, kaacha nyuma kasri moja kubwa
alililokuwa amejengea mpenziwe Michele ili wakaishi pamoja.
Mara yake ya kwanza kuja Afrika baada ya vita vya pili vya dunia,
Majununi kajenga hema na kasha kumwalika mpenziwe Michele. Kidosho huyo
kafika, akakataa katakata kushuka toka kwenye ndege na kumwambia
Majununi kwamba hawezi katu kuishi mwituni kama mnyama. Akaabiri ndege
na kurudi kwao Ufaransa. Kujenga nyumba yenye viumba vinne, Michele
kanengua kuwaq kamwe hawezi kuishi ndani ya kibanda. Majununi akawa
mtaftaji asiyechoka, ila akichoka, basi huwa keshapata. Kajenga basi
kasri kubwa lenye viumba kumi na vitatu. Asiyetosheka na la ninaye,
kumbe la mweziwe maradhi. Mara hii, kidosho kashuka na kuingia mle
kwenye kasri, vyumba kumi na vitatu? Bahati mbaya. Sakafu yenye rangi
nyekundu? Hatari, na mbona madirisha makubwa.
“Monsieur Noon, naomba radhi sana lakini hatufaani. Pengine imeandikwa
kwamba tusioane. Narudi kwetu. Katafute mwanamke kufu yako.” Ndiyo
maneno yake Michele kabla ya kuabiri ndege na kurudi kwao.
Akakosa
hata tone moja la mahaba rohoni kwa wanawake wote Majununi, na kasha
kaingilia ukulima na ufugaji kwa moyo, acha roho. Hata hivyo kwenye
bamba la zege karibu na dohani ukumbizoni kaandika, “Your beauty is my
weakness”, maneno yaliyobaki kuwa ukumbusho kwake kuhusu mapenzi yake
kwa Michele.
Mteni Nasaba akiwa kwenye Wizara ya Ardhi kajitengenezea stakabadhi
alizozitumia kunyakua shamba la mwajiri wake. Akawa Mtemi, mkubwa, nusu
mungu sijui nini. Watu wakawa ni kufyata ndimi dhidi ya dhulma zake
Mtemi. Akawa wa kuvunja wale waliodhubutu kumpinga na kuckichukua
akitakacho. Kwake hoja ikawa kupata alichokitafuta, wala si jinsi ya
kukipata.
Kwake Mtemi usafi zaidi kukawa balaa. Vitu vikuukuu, hela
hatumii hajali. Machweo wakafika akina Amani kwa Mtemi. Wakampata
kamsimamia fundu aliyekuwa akibambanyabambanya katika injini. Kawatupia
jicho la dharau na kuwauliza maswali za upumbavu. Akawakodolea macho na
kushangazwa na jawabuye Imani, aliyemtizama kwa kumkazia macho Mtemi
havumilii. “Usinivue nguo kwa macho yako wee!” (uk 21).
Akawaaga baada ya kumsukuma kidogo, eti aenda “kusukuhisha mgogoro wa shamba…” (uk 21). Akatokomea hukoo!
Basi
DJ kamfikisha Amani kwa Bi Zuhura, mkewe Mtemi Nasaba Bora. Amani akawa
akisubiri kuonyeshwa makazi yake, kwenye kibanda la wafanyikazi, la
makabwela kama yeye. Kufuka nje kwa Imani na DJ, jibwa lile jeupe,
aliyedhoofika na kung’ookang’ooka ngozi haliachi “kubweka bwe bwe, bweka
ubweke kufa kwaja.” (uk 24) akamwonea huruma DJ na kuuliza kwa nini kwa
nini lisiachwe “free maze”.
Akakumbushwa na Bi Zuhura asiwe “kama
wazungu wanaopaswa kukumbushwa kwamba mbwa ni ni mnyama”. Kukawa tayari
kumeingia machweo walipotoka akina DJ.
0 comments:
Post a Comment