SURA YA NANE
Ikuluni kwa Matuko Weye kaja askari mmoja na redio
aliyoitazamia kusikiliza matangazo ya mpira baina ya timu za Songoa FC
na Meza Wembe kutoka Wangwani. Wakawa wote, askari na waziri, Amani na
Imani wanayasikiliza matangazo hayo kwa njia mwafaka kabisa.
Mpira
karibu kumalizika, Songoa ikabahatika bao moja kutoka kwa mchezaji mmoja
maarufu kwa jina la Chwechwe Makweche almaarufu “Horsepower”. Imani
akajikuta katikati ya fahamu, hajui amshangilie kakake kwa kuifunia
Tomoko ama ahuzunike kwa kakake kuwasahau kabisa.
Kidogo kukasikika
mngurumo wa gari. Mtemi Nasaba kafika na kuwaamuru askari, “Wafungulieni
hawa washenzi watoke.” (uk 109). Wakawa huru Amani na Imani. Lakini
tujiulize, kwa nini wakaachwa huru bila kushtakiwa? Ndio wanyonge
hupitia, wasio na lao, hawana mbele wala nyuma.
Kuondoka kwake
Majisifu kuelekea Wangwani kulisadifiana na kurudi kwake Madhubuti
kutoka Urusi. Huku Amani na Imani wamesharudi kazini, Amani akatunga
beti kuhusu mwanawe wa kupanga, Uhuru. Baadaye akajaribu kutunga
nyingine kwa heshima ya rafikiye DJ, akashindwa, kwani maneno hayakuitwa
yakaitika. Twaona kwamba DJ kafikishwa zahanati ya Nasaba Bora baada ya
hali yake kuwa mbaya, huku adinda kunengua kilichokuwa kimemsadiki.
Miaka
mingi baadaye Imani kamsihi Amani iiandike tawasifu kuhusu maisha yake,
hakukosa kudukia yaliyomo baina yake na Madhubuti. Walikuwa masahibu wa
chanda na pete, hata wengi walishangazwa alipohamia Madhubuti kibandani
mwake Amani.
Wakawa wamepatana. Madhubuti akiwa tayari kwa mapinduzi
naye Amani akiwa tayari kupiga jeki. Mtemi haelewi yaliyomkuta mwanawe.
Madhubuti alipoajiriwa Songoa, wakawa wanawasiliana kupitia nyaraka.
Madhubuti akawa marafiki na maofisa wa wizara ya ardhi kwa lengo la
kupasua mbarika alikotokea Mtemi kumiliki mashamba mengi na makubwa
makubwa kama vile.
Tangu Mashaka kupata barua toka kwa Ben Bella, akawa “mnuni,kama kondoo”
(uk 121). Aliathiriwa sana na yale yawapatayo waliowachana kimapenzi.
Akakatiza masomo na kurudi nyumbani. Juhudi za wazaziye kumsihi akarudi
skulini zikaambulia patupu, mtoto akawa kisiki hasikii.
Majisifu naye
akafika chuo kikuu cha Mkokotoni kulikojaa sisisi, macho kama elfu za
na zaidi. Akakaribishwa na kasha kupewa nafasi akahutubu. “…alikumbwa na
kiherehere na kohoro.” (uk ) Ahaa! Mambo yanamwendea zegemnege.
Akafungua mkoba wake huku kijasho chembamba kinamtoka. Akaangusha
karatasi zake kutokana na uoga na kiwewe. Akarudi na kuketi chini huku
umati ukiangua kicheko.
Baada ya mhadhiri mmoja kunong’onezana naye
kwa muda, ikasemekana kwamba hangeweza kuhutubu moja kwa moja, basi
ikabidi wahadhiri waulize maswali huku Majisifu akiyajibu. Akaulizwa kwa
nini akachagua anwani “Kidagaa Kimemwozea” kwenye kitabu chake. “Kwa
kweli sijui ee, sijui kwa nini nilchagua kukiita kitabu hicho, Kidagaa
Kimemwozea. Niligutuka tu nimekiita hivyo.” (uk 123)
La pili akaulizwa maoni yake kuhusu jinsi mataifa ya Afrika baaada ya
mkoloni. “Kuna umoja na utangamano humu barani. Viongozi wa Afrika huru
wameshika usukani kwa njia bora zaidi. Afrika imekombolewa toka kwa
matatizo ya njaa, umaskini na ujinga.” (uk 123-124)
Akajikuta hawezi
kujibu maswali kwani majibu yake yalitfautiana sana na maoni yake kwenye
“Kidagaa Kimemwozea”. Akajitetea, “La! Mimi sikuonyesha hivyo kamwe
katika riwaya hiyo.” (uk ). Basi nani kaonyesha, na hata hivyo,
yanaonekana hata Mwalimu Majisifu hakuwa amekisoma kitabu hicho.
Wahadhiri
wakashangazwa hadi ya kushangazwa. Swali akalipata kuhusu hali ya
Kiswahili. Akajibu, “Kiswahili kitaendelea kuimarika vyema lakini sharti
tuondoe Watanzania na Wakenya kwenye ulingo…Watanzania wanadhania
kwamba ni wao tu ndio wakijua Kiswahili na Wakenya wanafikiria kwamba
kulipua makombora ya misamiati…” (uk 125) Kukalipuka kicheko.
Akaulizwa
ikiwa kaandika riwaya ya “Kidagaa Kimemwozea” na kwamba kulikuwa na
fununu kuwa kauchukua mswada wa mtu mwingine. “hayo yalikuwa mno.” (uk
125) Akafyata ulimi, huku unga umemzidi maji. Hata hivyo akaokolewa na
mhadhiri mmoja aliyedai kuwa hotuba ingeendelea siku iliyofuatia.
Jioni
hiyo, Majisifu akaabiri ndege kurudi Tomoko huku yu tayari kulipa fidia
ikibidi. Akajikuta “atokwa na machozi kama mtoto mdogo.” (uk 127)
Akajuta Majisifu, kumbe kidagaa kilikuwa kimemwozea.
0 comments:
Post a Comment