Sunday, February 7, 2016

KIDAGAA SURA YA SABA

SURA YA SABA
Siku tatu baada ya Mtemi kupokea barua kutoka kwa mwanawe Madhubuti, majira ya saa tatu asubuhi, kakake Mwalimu Majisifu akamtembelea kwake katika kasri la Majununi. Kukawa siku hizi, mkewe Bi Zuhura katafunwa na jakamoyo na upweke juu ya mumewe asiyesemezeka wala kuambilika. Kukawa Mtemi hawezichelewa kusuluhisha migogoro ya mashamba yake yasiyoisha.
Majisifu akapokelewa na Bi Zuhura wakawa wanapiga gumzo sebuleni. Alipotoka kukoga Mtemi, akavalia kwa muda, hajali kumsabahi. Baadaye akajitosa ukumbini aliposikia kakake kaulizia aliko. Bi Zuhura akawapa nafasi baada ya Mtemi kukaa mbali sana na wote wawili, Majisifu na Zuhura. Kimya kirefu kikajiri baina yao.
Alipojirudisha Mtemi, akamwuliza kakake majisifu kwa nini kakosekana mkutanoni. Majisifu naye akajibu kwamba kawa ameenda “ibada”. Akamwonya kakake Mtemi kuhusiana na madhara ya pombe, sana ikilinganishwa na vile baba yao kasisi kawakuza. Kujitetea majisifu akadai kwamba uovu uliofichwa ndani ya dini haumpendezi. “Afadhali nitende mambo yangu waziwazi.´(uk 93)

Mtemi akawa anampozoa Mwalimu hasira huku anajizuia kupasuka. Alipodai kujali maslahi yake Majisifu, akamwambia ajali maslahi ya Wanasokomoko wote. “Kama ungekuwa unajali maslahi yaw engine, yule mchungaji wako na mtumishi wangu hawangekuwa wanapigwa na baridi kule ndani kwa kosa ambalo hawakulitenda.” (uk )
Chai ilipoletwa mezani, Mtemi akashangaa kuona ni ya mkandaa. Akawa hana jingine ila kuinywa ili kuficha ukweli. Ndipo akagundua ndani mna nzi mkubwa wa buluu, kakufia mle ndani. Twaona kwamba haya yote ya suintofahamu katokana na kitiwa kwa Amani mbaroni. Wakawa hawaongezani wala kusemezana. Kukawa kimya.
Yalipozidi unga, Majisifu akaaga na kutokomea mbali, ukuta wa uhasama ukakithiri baina yao. Lakini kitu kimoja walichokosa kujua ni kwamba siku hiyo kawa mwisho wa kukutana kwao katika kasri la Majununi. Hatujui kukatokea nini baadaye ila tu tusome. Kutoka kwake Mtemi bila kwaheri, Majisifu akahesabu boriti kuelekea kwa Mama N’tilie alikotarajia kuwa na ibada.
Akakumbuka kwamba alikuwa na kipindi kimoja cha kufundisha lakini akadai kuwapa nafasi wale maziwa lala wakawaandikie muhibu wao barua za mapenzi na kupanga jinsi ya kukiuka vizingiti vya shule.
Hapa twajagundua kwamba Mwalimu Majisifu hakuwa na akili nzuri ya kumwezesha kuandika vitabu. “Ningekuwa na akili nzuri ya kuandika kitabu ningeandika juu ya kibe wachezacho wasichana hao na mwalimu mkuu…” (uk 98)

Akaitisha bibilia Mtemi na kuanza kusoma, kitu alichokawia kufanya miaka nenda miaka rudi. Akakumbuka kuhusu kidoshao kimoja kiguru aliabiri naye gari pamoja kuelekea mjini. Akajitetea Nasaba lakini kakosolewa kwamba hangeweza kucheza ngoma ile hata kama ni yeye aliyeianzisha. Kutia nanga mjini, Nasaba akamwona Yule mrembo akiinama na kutoa mikongojo miwili ya kwapani. Akagundua ukweli, upendo ukamtoka, akaomba radhi na kutokomea.
Na katika harakati hizi ndipo kukasikika ukwenzi mkali kutoka nje. Alipotazama Zuhura ili kutendua kilichosadiki, akamwona DJ yu chini huku mguu wake uking’atwa na mbwa Jimmy. Zuhura akamcharaza Yule mbwa na akatoroka asionekane tena. Akampokeza barua ile Bi Zuhura na kuomba kuondoka ili kupeleka ng’ombe wa mwajiri wake malishoni.
Basi mkewe Mtemi akamfikishia barua yake, hapo ndipo pakatokea mzozano baina yao Zuhura alipomwonya Mtemi kwa kutowachanja mbwa wake wakti akiwahukumu wale waliokosa kuwachanja wao. Kwa madharau akadai kwamba DJ alistahili alichokipata.
Kufungua barua ile, akakutana na yalimshangaza. Lowela akaonya kutoboa siri Mtemi akosapo kuwaachilia huru Amani na Imani. Ndiyo mapenzi ya masharti yake binti wa watu. “Moyo ulimpapa na kijasho chembamba juu ya mwanzi wa pua. Akahisi uchungu wa mwiba wa kujidunga.” (uk 106) Atahadhari huku maji yashammwagikia? Nani atakayeyazoa?
Share:

0 comments:

Post a Comment

Popular Posts

Unordered List

Pages

Categories

Labels

Download

Powered by Blogger.

Footer Widget 1

Text Widget

Blogger Tricks

Blogger Themes

Categories

Copyright © MWONGOZO NA UCHAMBUZI WA FASIHI ANDISH | Powered by Jkts Company 0706509638 |