Sunday, February 7, 2016
MWONGOZO WA KIDAGAA SURA YA KWANZA
SURA YA KWANZA
Chini ya mti mmoja kando yam to Kiberenge, vijana wawili, amani na Imani wanapunga hewa baada ya kukata kiu. Aidha, wamo safarini kuelekea Sokomoko, kila mmoja na haja yake. Kitambo kidogo tu, wawili hawa wamevunja mwiko kwa kuyanywa maji yam to kiberenge ambao wenyeji wanaamini kuwa haramu.
Muda si kitambo, wenyeji hawachelewi kuambizana na kusimuliana juu ya waja wawili, waliovunja mwiko kwa kuyanywa maji haramu ya Kiberenge na wakakosa kuaga dunia. Kwa kweli, wakati mwingine haramu huweza kuhalalishwa kulingana na watendwa. Imani anayo imani kwamba hakuna haja yoyote ya kuogopa kutenda bila kujaribu.
Ni katika harajkati hizi za kukata kiu ndipo wanapokutana na vijana wanaokoga na kupiga mbizi mtoni. Wakti huu,mifugo ya matajiri wanala nyasi baada ya kujitosheleza kwa maji.
Fahali mmoja mweusi anaizoa kinywani suruali moja kuukuu linalomilikiwa na na kijana mmmoja mneni sana. Wanapogundua linalojiri baada ya kufahamishwa na Imani, vijana wale wanaparamia ukingoni na kuanza kumfukuza Yule fahali lakini wapi, anaposimama, suruali keshaimeza tumboni.
Ndilo vazi la kipekee alilokuwa nayo DJ, kwikwikwi na msononeko zikamkaba yule kijana hohehahe asiye na mbele wala nyuma. Jahazi linaokolewa na Amani anapofungua mkoba wake na kutoa shati moja, akamwita kijana yule na kumpoza shati.
Kwa kuwaamini wageni hawa wasiojulikana kutoka kwao, DJ anawasimulia yaliyomjiri. Kazaliwa na kukuzwa na mama mmoja mpishi wa pombe haramu mtaani Madongoporomoka mjini Songoa. Kasingiziwa kuiba na kufungwa jela ya watoto anakotoroka na ndipo kufika Sokomoko anakoajiriwa na mkewe Maozi kama mmoja wa familia.
Hatimaye, wanaandamana kuelekea Sokomoko ambako DJ awaelekeza kwa ndugu wawili matajiri, Mtemi Nasaba Bora anayehitaji mchungaji ilhali kakake Mwalimu Majisifu anahitaji kijakazi. Njiani, anawatahadharisha kuhusu udhalilishaji na mishahara duni ambazo wangekumbana nazo.
Hapa ndipo Amani kategua siri kadhaa zikiwemo kutafuta njia yakumwokoa amu yake na kufichwa kwa mali ya nasaba yake. Kajitayarisha kukumbana na mahasimu wake, bila dhamira ya kulipiza kisasi. Imani naye kafika kwa kukosa pa kuenda baada ya mastakimu yake kuteketezwa na wasiojulikana. Amani ana umri wa miaka ishirini naye Imani kumi na minne
Wakti huu, Mashaka anapata nafasi ya kupenya na kuingia umatini anapokutana na mpenziye Ben Bella. Tunamwona Bella akimkabidhi mashaka barua na kasha Mashaka kutokomea msalani. Mvua inaanza kunyesha baada ya Mtemi kumaliza hotuba yake aliyoitoa kwa lugha ya kimombo ambapo, “kila mtu alihisi kugeuzwa…akawa bumbumbu mzungu wa reli”. (uk 70)
Watu wanajaribu kujisetiri ndani ya hema aliko Mtemi na aila yake ili kuepuka mvua lakini “wanazuiliwa na Askari kwa amri ya Mtemi”. Yanapomzidi matuko Weye , anakwea jukwani na kukamata kipaza sauti. Anayabwaga yaliyo rohoni, machungu yanayomkereketa nyongo na kumshambulia Mtemi kwa ubaradhuli, unyanyasaji, dhulma na wizi. Anatunyang’anya mashamba, mali, mabinti na hata wake zetu wenyewe.” (uk 71)
DJ anamfahamisha Amani kuhusu ugonjwa wa mtoto Uhuru. Amani anajitokeza kuelekea kibandani kwake huku akicharazwa na mvua. Muda si mwingi, gari la Mtemi Nasaba linavuma na analipisha amani, gari hili ambalo lilimpita mwanamke aliyekuwa akijifungua njiana alipotoka mkutanoni.
Amani na Imani wanaandamana kuelekea zahanati ya Nasaba Bora ili angalau motto Uhuru akapate kutibiwa. “Walipofika si mabezo hayo waliyofanyiwa na wauguzi wa kike waliokuwa wanafuma fulana zao na kupiga zohali.” (uk 76) Nashangazwa sana nay ale yanayoendelea katika vituo na maofisi za serikali tunakotarajia wananchi kuhudumiwa. Ni wangapi waliowahi kuaga dunia kutokana na vituko vya madaktari na wauguzi? Kitambo si sana, nduguye Imani kaaga, leo hii ni motto Uhuru asiye na hatia. Asiyewahi kutenda maovu yoyote.
“Maisha ni mshumaa usiokuwa na mkesho.” (uk 78) Ndivyo alivyonena amani baada ya kitoto Uhuru kulala usingizi usiokuwa na mkomo. Hata hivyo Imani hakuweza msahau kitoto kile cha kupagazwa, basi alipompata mtotowwe, basi akaamua kukiita kindakindaki Uhuru wa Pili.
0 comments:
Post a Comment