SURA YA TANO
Uwanja wa Nasaba Bora ambapo wananchi wansherehekea
sikukuu ya Wazalendo umefumukana hadi ya kufumuka. Wameroa kwa jasho
kutokana na joto jingi. Waliomo, wananchi wa kawaida hawakuchelewa
kufika, saa tatu upuzi walikuwa wamefika. Acha viongozi waje wakti wao
na kufika pao, walipotengewa.
Mwendo wa saa tano unusu, anafika Mtemi
na aina yake. Jukwani anapanda Balozi, jamaa mcheshi na mjanja. Anayo
matamu matamu yanayoweza kumtoa nyoka pangoni. Hata hivyo, anajihadhari
asije akaukate “mkono uliokuwa ukimlisha au kuziuma chuchu
alizozinyonya”. (uk 67)
Ingawa Balozi ni mtu aliye na ushawishi
mkubwa kwa umati, hakosi kuonyesha uzembe wake kwa kumsifu Mtemi, sifa
zilizo kinyume kabisa na matendo yake Mtemi Nasaba Bora. Anapowauliza
wananchi ikiwa kunaye yeyote asiyempenda Mtemi, kimya kinawazidi
wasiweze hata kohoa. “Anatambulikana kwa fadhili na utu wema
wake…Kiongozi aliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu.” (uk 68) Angurumapo samba,
mcheza nani? Hakuna aliyethubutu ila wengine kama Mzee Matuko Weye.
Hata hivyo hatukosi wale wa kunung’unika kichichini angalau wasije
wakapatikana na Askari wake Mtemi, Bi Kizee akiwemo.
0 comments:
Post a Comment