MASWALI
1. Je kuna umuhimu gani wa hadithi ndani ya hadithi kama ilivyotumika katika riwaya ya “Kidagaa Kimemwozea”?
2. Eleza jinsi riwaya ya Kidagaa Kimemwozea ilivyoakizi jamii halisi ya Kenya ya sasa.
3. Eleza matatizo yanayowakumba vijana kwenye riwaya ya Kidagaa kimemzea.
4. Thibitisha maudui ya ufisadi katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
5. Eleza jinsi maudhui yaq uteleleshi imejitokeza katika riwaya ya Kidagaa kimemwozea.
6. Eleza athari za ukoloni mamboleo.
7. Kidagaa kimemwozea ni anwani inayodokeza kuharibikiwa kwa mambo. Jadili ukweli wa kauli huu.
8. Ukengeushi ni mojawapo ya matatizo yanayozikumba jamii za Afrika. Thibitisha kwa kurejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
9. Eleza jinsi mbinu ya majazi imetumika katika riwaya ya Kidagaa kimemwozea.
10. Mbinu ya kinaya imetumika vipi katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. Thibitisha.
11. Pana mbinu ya ishara katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. Itambue ishara hiyo na kueleza inachoashiria.
12. Taja na ufafanue mifano miwili ya methali iliyotumiwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
13. Taja sifa mbili za Mtemi Mtemi Nasaba bora ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
14. Eleza jinsi mbinu ya taharukiimejitokeza katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
15. Anwani ya Kidagaa Kimemwozea ingeweza kuitwa Songoa. Jadili kwa kutoa mifano mwafaka.
16. Mbinu ya utabiri imetumikajae katika riwaya hii iliyosukwa ikasukika?
17. Eleza jinsi kiangaza mbele ilivyotumika katika riwaya hii.
18. Uwendawazimu wa Weye si uwendawazimu tu! Bali kuna ukweli na uhakika fulani ndani yake. Jadili.
19. Taja na ufafanue wahusika waliozewa na kidagaa.
20. Eleza sababu ya Amani kutupa mswada ziwani.
21. Amani na Madhubuti wanaleta mwamko mpya katika eneo la Sokomoko. Thibitisha.
22. Jazanda imejitokeza vipi katika riwaya hii?
23. Kidagaa ni nini na kimemwozea nani?
b) Toa sababu ya kidagaa kuoza.
24. “Mgalla muue na haki umpe.”
a) Eleza muktadha wa dondo hili.
25. “Hakuna refu lisilokuwa na ncha.”
a) Elezea ufaafu wa methali hii ukirejelea maisha ya Mtemi Nasaba Bora.
26. “Sijawahi ona kibogoyo akiguguna mifupa, waweza andika nini wewe?”
a) Lihakiki dondoo hili.
27. “Nimekuwa ganda la mua”.
a) Eleza muktadha wa dondo hili.
b) Anayelengwa na maneno haya amekua ganda la mua. Fafanua.
c) Jadili kuharibikiwa kwa wahusika hawa.