Sunday, February 7, 2016

MASWALI YA KIDAGAA KIMWOZEA


MASWALI
1.           Je kuna umuhimu gani wa hadithi ndani ya hadithi kama ilivyotumika katika riwaya ya “Kidagaa Kimemwozea”?
2.           Eleza jinsi riwaya ya Kidagaa Kimemwozea ilivyoakizi jamii halisi ya Kenya ya sasa.
3.           Eleza matatizo yanayowakumba vijana kwenye riwaya ya Kidagaa kimemzea.
4.           Thibitisha maudui ya ufisadi katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
5.           Eleza jinsi maudhui yaq uteleleshi imejitokeza katika riwaya ya Kidagaa kimemwozea.
6.           Eleza athari za ukoloni mamboleo.
7.           Kidagaa kimemwozea ni anwani inayodokeza kuharibikiwa kwa mambo. Jadili ukweli wa kauli huu.
8.           Ukengeushi ni mojawapo ya matatizo yanayozikumba jamii za Afrika. Thibitisha kwa kurejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
9.           Eleza jinsi mbinu ya majazi imetumika katika riwaya ya Kidagaa kimemwozea.
10.        Mbinu ya kinaya imetumika vipi katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. Thibitisha.
11.        Pana mbinu ya ishara katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. Itambue ishara hiyo na kueleza inachoashiria.
12.        Taja na ufafanue mifano miwili ya methali iliyotumiwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
13.        Taja sifa mbili za Mtemi Mtemi Nasaba bora ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
14.        Eleza jinsi mbinu ya taharukiimejitokeza katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
 15.        Anwani ya Kidagaa Kimemwozea ingeweza kuitwa Songoa. Jadili kwa kutoa mifano mwafaka.
16.        Mbinu ya utabiri imetumikajae katika riwaya hii iliyosukwa ikasukika?
17.        Eleza jinsi kiangaza mbele ilivyotumika katika riwaya hii.
18.        Uwendawazimu wa Weye si uwendawazimu tu! Bali kuna ukweli na uhakika fulani ndani yake. Jadili.
19.        Taja na ufafanue wahusika waliozewa na kidagaa.
20.        Eleza sababu ya Amani kutupa mswada ziwani.
21.        Amani na Madhubuti wanaleta mwamko mpya katika eneo la Sokomoko. Thibitisha.
22.        Jazanda imejitokeza vipi katika riwaya hii?
23.        Kidagaa ni nini na kimemwozea nani?
b) Toa sababu ya kidagaa kuoza.
24.        “Mgalla muue na haki umpe.”
a)            Eleza muktadha wa dondo hili.
25.        “Hakuna refu lisilokuwa na ncha.”
a)            Elezea ufaafu wa methali hii ukirejelea maisha ya Mtemi Nasaba Bora.
26.        “Sijawahi ona kibogoyo akiguguna mifupa, waweza andika nini wewe?”
a)            Lihakiki  dondoo hili.
27.         “Nimekuwa ganda la mua”.
a)            Eleza muktadha wa dondo hili.
b)           Anayelengwa na maneno haya amekua ganda la mua. Fafanua.
c)            Jadili kuharibikiwa kwa wahusika hawa.

Share:

KIDAGAA SURA YA TISA

SURA YA TISA
Alidhania hawezi kufa hata alipowadhalimu na kuwatesa wananchi wasio na hatia. Akaanza kupanga mazishi yake huku ajihisi marehemu. Siku moja kamwita Amani na kumpa sururu, jembe na sepetu. “nataka uchimbe hapa kaburi langu. Siku nitakapokufa nataka kuzikwa hapa.” (uk 128) Ingawa Amani hakulitegemea, akawa hana budi ila kukamilisha jukumu lake. Hivyo basi, akalichimba kaburi hilo kwa siku tatu, likawa la fahari.
Mashaka kwake kukawa mashaka kweli, habebeki mwana wa watu. “Abwajabwaja ovyoovyo kama Mzee matuko Weye. (uk 129) Masomo keshaikatiza, nguo katupa na kuzura tupu mitaani. “Kumbe chema hakidumu.” (uk 129) Madhubuti amejitolea kutumikia nchi yake kwa moyo wake wote, tendo lililokuwa mkabala na alivyoamini baba mtu. “…alielewa fika kwamba ingebidi aukate mkono uliokuwa ukimlisha tangu hapo hata matokeo yake yakiwa nini.” (uk 130)
Mashaka akaleta rabsha na kuwazidi wafanyikazi wengine. Bi Zuhura akamwita Amani na pamoja wakamfungia Mashaka chumbani mwake. Kwa kuogofya yaliyokuwa yakiendelea, Bi Zuhura akamsihi Amani kalale ukumbini. Nyakti za usiku, Amani akaitwa na Bi Zuhura ili kaangalie ni nini kilichokuwa chini ya kitanda chake mama mtu. Ni katika harakati hizi ndipo Bwana Mtemi akarejea na kuwakuta wawili chumbani, wanatetemeka. “Ndani kukawa hakukaliki, nje hakutokeki.” (uk 131) “Kumbe huyu mwanamke huniendea kinyume na mfanyikazi jamani?” (uk 131) Akafungua sefu Mtemi, akatoa bunduki na kumshambulia. Alipodiriki kwamba Amani kaaga dunia, akambeba kwenye buti ya gari lake na kumtupa kando yam to Kiberenge, ambako aliokotwa na Wasamaria wema na kupelekwa zahanati ya Nasaba Bora.

Kukawa siku nyingi zimepita Amani akiwa zahanatini. Alipofumbua macho na kisha kuachwa huru, Imani wakaambatana na Majisifu kumpeleka kwake Majisifu mwenyewe. Amani kufika nyumbani, akakubaliwa kukaa katika “servants quarters” huku bado hawezi kuongea na kuwasiliana kwa kuandika. Imani akamchunga kakake vizuri sana.
Amani akamfahamisha Imani ya kuwa angependa kujistarehesha kwa kusoma vitabu. Imani akamwazimia vitabu kutoka kwa Mwalimu Majisifu, ikiwemo kimoja kwa anwani la “Kidagaa kimemwozea”. Kwa mshangao, kitabu chenye picha ndicho kile chake, mswada aliyorudishiwa kwa kuwa hauwezi chapika. Majisifu kajikuta taabani. “Lililomshangaza ni kwamba Yule aliyeitwa mwandishi na kupachikwa picha yake katika jalada la nyuma, hakuwa ndiye mwandishi wa kitabu hicho.” (uk 140) “…kilichokuwa chake kimekuwa cha mwingine.” (uk 141)
Amani akamwandikia Imani barua kumwelezea juu ya le aliyoyaona. Majisifu akaipata barua ile na kuisoma. Hapo Imani akampata na kumkabili vipasavyo. Majisifu akatoa zote siri alizokuwa amezibana, “Kumbe umdhaniye ndiye siye?” Akamwandikia karatasi ndogo Amani kwa Majisifu.
Share:

KIDAGAA SURA YA NANE

SURA YA NANE
Ikuluni kwa Matuko Weye kaja askari mmoja na redio aliyoitazamia kusikiliza matangazo ya mpira baina ya timu za Songoa FC na Meza Wembe kutoka Wangwani. Wakawa wote, askari na waziri, Amani na Imani wanayasikiliza matangazo hayo kwa njia mwafaka kabisa.
Mpira karibu kumalizika, Songoa ikabahatika bao moja kutoka kwa mchezaji mmoja maarufu kwa jina la Chwechwe Makweche almaarufu “Horsepower”. Imani akajikuta katikati ya fahamu, hajui amshangilie kakake kwa kuifunia Tomoko ama ahuzunike kwa kakake kuwasahau kabisa.
Kidogo kukasikika mngurumo wa gari. Mtemi Nasaba kafika na kuwaamuru askari, “Wafungulieni hawa washenzi watoke.” (uk 109). Wakawa huru Amani na Imani. Lakini tujiulize, kwa nini wakaachwa huru bila kushtakiwa? Ndio wanyonge hupitia, wasio na lao, hawana mbele wala nyuma.
Kuondoka kwake Majisifu kuelekea Wangwani kulisadifiana na kurudi kwake Madhubuti kutoka Urusi. Huku Amani na Imani wamesharudi kazini, Amani akatunga beti kuhusu mwanawe wa kupanga, Uhuru. Baadaye akajaribu kutunga nyingine kwa heshima ya rafikiye DJ, akashindwa, kwani maneno hayakuitwa yakaitika. Twaona kwamba DJ kafikishwa zahanati ya Nasaba Bora baada ya hali yake kuwa mbaya, huku adinda kunengua kilichokuwa kimemsadiki.
Miaka mingi baadaye Imani kamsihi Amani iiandike tawasifu kuhusu maisha yake, hakukosa kudukia yaliyomo baina yake na Madhubuti. Walikuwa masahibu wa chanda na pete, hata wengi walishangazwa alipohamia Madhubuti kibandani mwake Amani.
Wakawa wamepatana. Madhubuti akiwa tayari kwa mapinduzi naye Amani akiwa tayari kupiga jeki. Mtemi haelewi yaliyomkuta mwanawe. Madhubuti alipoajiriwa Songoa, wakawa wanawasiliana kupitia nyaraka. Madhubuti akawa marafiki na maofisa wa wizara ya ardhi kwa lengo la kupasua mbarika alikotokea Mtemi kumiliki mashamba mengi na makubwa makubwa kama vile.

Tangu Mashaka kupata barua toka kwa Ben Bella, akawa “mnuni,kama kondoo” (uk 121). Aliathiriwa sana na yale yawapatayo waliowachana kimapenzi. Akakatiza masomo na kurudi nyumbani. Juhudi za wazaziye kumsihi akarudi skulini zikaambulia patupu, mtoto akawa kisiki hasikii.
Majisifu naye akafika chuo kikuu cha Mkokotoni kulikojaa sisisi, macho kama elfu za na zaidi. Akakaribishwa na kasha kupewa nafasi akahutubu. “…alikumbwa na kiherehere na kohoro.” (uk ) Ahaa! Mambo yanamwendea zegemnege. Akafungua mkoba wake huku kijasho chembamba kinamtoka. Akaangusha karatasi zake kutokana na uoga na kiwewe. Akarudi na kuketi chini huku umati ukiangua kicheko.
Baada ya mhadhiri mmoja kunong’onezana naye kwa muda, ikasemekana kwamba hangeweza kuhutubu moja kwa moja, basi ikabidi wahadhiri waulize maswali huku Majisifu akiyajibu. Akaulizwa kwa nini akachagua anwani “Kidagaa Kimemwozea” kwenye kitabu chake. “Kwa kweli sijui ee, sijui kwa nini nilchagua kukiita kitabu hicho, Kidagaa Kimemwozea. Niligutuka tu nimekiita hivyo.” (uk 123)

La pili akaulizwa maoni yake kuhusu jinsi mataifa ya Afrika baaada ya mkoloni. “Kuna umoja na utangamano humu barani. Viongozi wa Afrika huru wameshika usukani kwa njia bora zaidi. Afrika imekombolewa toka kwa matatizo ya njaa, umaskini na ujinga.” (uk 123-124)
Akajikuta hawezi kujibu maswali kwani majibu yake yalitfautiana sana na maoni yake kwenye “Kidagaa Kimemwozea”. Akajitetea, “La! Mimi sikuonyesha hivyo kamwe katika riwaya hiyo.” (uk ). Basi nani kaonyesha, na hata hivyo, yanaonekana hata Mwalimu Majisifu hakuwa amekisoma kitabu hicho.
Wahadhiri wakashangazwa hadi ya kushangazwa. Swali akalipata kuhusu hali ya Kiswahili. Akajibu, “Kiswahili kitaendelea kuimarika vyema lakini sharti tuondoe Watanzania na Wakenya kwenye ulingo…Watanzania wanadhania kwamba ni wao tu ndio wakijua Kiswahili na Wakenya wanafikiria kwamba kulipua makombora ya misamiati…” (uk 125) Kukalipuka kicheko.
Akaulizwa ikiwa kaandika riwaya ya “Kidagaa Kimemwozea” na kwamba kulikuwa na fununu kuwa kauchukua mswada wa mtu mwingine. “hayo yalikuwa mno.” (uk 125) Akafyata ulimi, huku unga umemzidi maji. Hata hivyo akaokolewa na mhadhiri mmoja aliyedai kuwa hotuba ingeendelea siku iliyofuatia.
Jioni hiyo, Majisifu akaabiri ndege kurudi Tomoko huku yu tayari kulipa fidia ikibidi. Akajikuta “atokwa na machozi kama mtoto mdogo.” (uk 127) Akajuta Majisifu, kumbe kidagaa kilikuwa kimemwozea.
 

Share:

KIDAGAA SURA YA SABA

SURA YA SABA
Siku tatu baada ya Mtemi kupokea barua kutoka kwa mwanawe Madhubuti, majira ya saa tatu asubuhi, kakake Mwalimu Majisifu akamtembelea kwake katika kasri la Majununi. Kukawa siku hizi, mkewe Bi Zuhura katafunwa na jakamoyo na upweke juu ya mumewe asiyesemezeka wala kuambilika. Kukawa Mtemi hawezichelewa kusuluhisha migogoro ya mashamba yake yasiyoisha.
Majisifu akapokelewa na Bi Zuhura wakawa wanapiga gumzo sebuleni. Alipotoka kukoga Mtemi, akavalia kwa muda, hajali kumsabahi. Baadaye akajitosa ukumbini aliposikia kakake kaulizia aliko. Bi Zuhura akawapa nafasi baada ya Mtemi kukaa mbali sana na wote wawili, Majisifu na Zuhura. Kimya kirefu kikajiri baina yao.
Alipojirudisha Mtemi, akamwuliza kakake majisifu kwa nini kakosekana mkutanoni. Majisifu naye akajibu kwamba kawa ameenda “ibada”. Akamwonya kakake Mtemi kuhusiana na madhara ya pombe, sana ikilinganishwa na vile baba yao kasisi kawakuza. Kujitetea majisifu akadai kwamba uovu uliofichwa ndani ya dini haumpendezi. “Afadhali nitende mambo yangu waziwazi.´(uk 93)

Mtemi akawa anampozoa Mwalimu hasira huku anajizuia kupasuka. Alipodai kujali maslahi yake Majisifu, akamwambia ajali maslahi ya Wanasokomoko wote. “Kama ungekuwa unajali maslahi yaw engine, yule mchungaji wako na mtumishi wangu hawangekuwa wanapigwa na baridi kule ndani kwa kosa ambalo hawakulitenda.” (uk )
Chai ilipoletwa mezani, Mtemi akashangaa kuona ni ya mkandaa. Akawa hana jingine ila kuinywa ili kuficha ukweli. Ndipo akagundua ndani mna nzi mkubwa wa buluu, kakufia mle ndani. Twaona kwamba haya yote ya suintofahamu katokana na kitiwa kwa Amani mbaroni. Wakawa hawaongezani wala kusemezana. Kukawa kimya.
Yalipozidi unga, Majisifu akaaga na kutokomea mbali, ukuta wa uhasama ukakithiri baina yao. Lakini kitu kimoja walichokosa kujua ni kwamba siku hiyo kawa mwisho wa kukutana kwao katika kasri la Majununi. Hatujui kukatokea nini baadaye ila tu tusome. Kutoka kwake Mtemi bila kwaheri, Majisifu akahesabu boriti kuelekea kwa Mama N’tilie alikotarajia kuwa na ibada.
Akakumbuka kwamba alikuwa na kipindi kimoja cha kufundisha lakini akadai kuwapa nafasi wale maziwa lala wakawaandikie muhibu wao barua za mapenzi na kupanga jinsi ya kukiuka vizingiti vya shule.
Hapa twajagundua kwamba Mwalimu Majisifu hakuwa na akili nzuri ya kumwezesha kuandika vitabu. “Ningekuwa na akili nzuri ya kuandika kitabu ningeandika juu ya kibe wachezacho wasichana hao na mwalimu mkuu…” (uk 98)

Akaitisha bibilia Mtemi na kuanza kusoma, kitu alichokawia kufanya miaka nenda miaka rudi. Akakumbuka kuhusu kidoshao kimoja kiguru aliabiri naye gari pamoja kuelekea mjini. Akajitetea Nasaba lakini kakosolewa kwamba hangeweza kucheza ngoma ile hata kama ni yeye aliyeianzisha. Kutia nanga mjini, Nasaba akamwona Yule mrembo akiinama na kutoa mikongojo miwili ya kwapani. Akagundua ukweli, upendo ukamtoka, akaomba radhi na kutokomea.
Na katika harakati hizi ndipo kukasikika ukwenzi mkali kutoka nje. Alipotazama Zuhura ili kutendua kilichosadiki, akamwona DJ yu chini huku mguu wake uking’atwa na mbwa Jimmy. Zuhura akamcharaza Yule mbwa na akatoroka asionekane tena. Akampokeza barua ile Bi Zuhura na kuomba kuondoka ili kupeleka ng’ombe wa mwajiri wake malishoni.
Basi mkewe Mtemi akamfikishia barua yake, hapo ndipo pakatokea mzozano baina yao Zuhura alipomwonya Mtemi kwa kutowachanja mbwa wake wakti akiwahukumu wale waliokosa kuwachanja wao. Kwa madharau akadai kwamba DJ alistahili alichokipata.
Kufungua barua ile, akakutana na yalimshangaza. Lowela akaonya kutoboa siri Mtemi akosapo kuwaachilia huru Amani na Imani. Ndiyo mapenzi ya masharti yake binti wa watu. “Moyo ulimpapa na kijasho chembamba juu ya mwanzi wa pua. Akahisi uchungu wa mwiba wa kujidunga.” (uk 106) Atahadhari huku maji yashammwagikia? Nani atakayeyazoa?
Share:

KIDAGAA SURA YA SITA

SURA YA SITA
Mashaka akafikishwa shuleni kwa gari la babake. Akakimbia hadi chumbani mwake na kujifungia. Akaitoa barua aliyoipata toka kwa Bella. Ndani akafahamishwa kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa kiushuhuba ulioko baina yao wawili; Mashaka na Ben Bella. Mtemi Nasaba Bora kampachika mimba mwana wa watu, Lowela dadake Bella. Basi Lowela kajifunga kamba tumboni hadi wakti wa kujifungua bila ya wazaziye kufahamu. Mtemi akamtorosha na kuficha Baraka alipopatikana na Ben na kuelezea yaliyotukia.
Wakati ambapo Ben Bella anachumbiana na Mashaka bintiye Mtemi Nasaba Bora, Mtemi naye anashuhubiana na Lowela mwanawe Bwana Maozi. Vipi ushemeji ukawezekana wakti baba na bintiye wanapendana na ndugu wawili wa damu moja? Ni uchafu na ukaidi gani tunaoupata hapa? Msomaji jiulize swali hili. Mtemi ni kiongozi mtukufu aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu, huku hakosi “kusuluhisha migogoro ya shamba” na kuvuna asipopalilia.
Asubuhi ya siku ya pili baada ya sikukuu ya Wazalendo, askari wakafika na kuwakabili akina Amani, waliodaiwa kumwua mtoto Uhuru, na tuhuma nyingine kuwa Imani kakosa kuhudhuria Uwanja wa Nasaba Bora kwenye sharehe.
Wakatupwa kwenye ikulu ya rais Matuko Weye, walikompata kapotea kwenye usingizi akoroma. Kelele zile za kujitetea kwa akina Amani na tani za askari zikamuamsha rais kutoka lepe lake la usingizi. “Miye mtukufu rais bado nalala na mwaniletea kelele?” (uk 85) Katika harakati za kuwakagua waziri alioletewa, wa ufisadi na magendo bora watoe kitu kidogo.
Akamwona msichana Imani. “Nenda ukaolewe weye ukazae watoto…wakaikomboe Tomoko toka kwa mkoloni mweusi.” (uk 85). Basi vituko na vitani hivi vikafikia kikomo kuliposikika ngurumo za gari la Mtemi. Kama kawaida, Yule askari mrefu akakimbia kulifungua lango la gari baada ya kupiga saluti.

Alipoketi ofisini mwake, akapokea barua na gazeti Mtemi. Akatizamatizama kwenye gazeti la Tomoko leo na kukosa picha yake. Akakumbuka kwamba kakake Majisifu alipokuwa mhariri wa gazeti lile, basi picha zake hazikukosekana ingawa kulikuwa na  suintofahamu baina yao. Kufungua barua ile iliyotoka kwa mwanawe Madhubuti akafahamishwa kwamba Madhubuti angeweza kurudi nyumbani mwishoni mwa mwezi ule. Hata hivyo Madhubuti akaonya kwamba asingependa kufanya kazi zipatikanazo kwa hongo na milungura. Yeye angependa kula jasho lake mwenyewe.
Mzee Matuko alipoamriwa toka ikuluni, akadinda huku akidai, “Lakini hata mkiniua kumbukeni kwamba watazaliwa Matuku wengine watakaoendelea na harakati za ukombozi toka pale nilipoachia.” (uk 86)
Akaghadhibika sana Mtemi kutokana na barua ile. Kwa hasira na hamaki, akaamuru akina Imani kupigwa na kuteswa. “Wale mahabusu mkwafanyie kazi kama kawaida.” (uk 88) Akaliweka gari moto kuelekea janibu nyumbani kwake. Wakti huo walipokuwa wakifanyiwa kazi, Amani alibaki kunyamaza tu kama kiumbe kisichokuwa na uhai huku Imani akipiga ukwenzi uliosikika mbali.





Share:

KIDAGAA SURA YA TANO

SURA YA TANO
Uwanja wa Nasaba Bora ambapo wananchi wansherehekea sikukuu ya Wazalendo umefumukana hadi ya kufumuka. Wameroa kwa jasho kutokana na joto jingi. Waliomo, wananchi wa kawaida hawakuchelewa kufika, saa tatu upuzi walikuwa wamefika. Acha viongozi waje wakti wao na kufika pao, walipotengewa.
Mwendo wa saa tano unusu, anafika Mtemi na aina yake. Jukwani anapanda Balozi, jamaa mcheshi na mjanja. Anayo matamu matamu yanayoweza kumtoa nyoka pangoni. Hata hivyo, anajihadhari asije akaukate “mkono uliokuwa ukimlisha au kuziuma chuchu alizozinyonya”. (uk 67)
Ingawa Balozi ni mtu aliye na ushawishi mkubwa kwa umati, hakosi kuonyesha uzembe wake kwa kumsifu Mtemi, sifa zilizo kinyume kabisa na matendo yake Mtemi Nasaba Bora. Anapowauliza wananchi ikiwa kunaye yeyote asiyempenda Mtemi, kimya kinawazidi wasiweze hata kohoa. “Anatambulikana kwa fadhili na utu wema wake…Kiongozi aliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu.” (uk 68) Angurumapo samba, mcheza nani? Hakuna aliyethubutu ila wengine kama Mzee Matuko Weye. Hata hivyo hatukosi wale wa kunung’unika kichichini angalau wasije wakapatikana na Askari wake Mtemi, Bi Kizee akiwemo.
Share:

KIDAGAA SURA YA NNE

                                     SURA YA NNE
“Siku tatu tangu Imani kende kwa nduguye nab ado hajaonekana.” (uk 49) Dora hakuweza kuvumilia kuwa linda wanawe. Akazidiwa hamaki na kumshambulia mumewe Bwana Majisifu ambaye kajibu kwa “kumfungulia cherehani ya matusi” (uk 52).
Hata hivyo, majibizano hayo yanakatizwa ghafla mlango unapobishwa na mpwa wake majisifu, Mashaka bintiye Mtemi Nasaba Bora. Majisifu na Dora wanavua nyuso za hasira na  kujibandika za bashasha, anagalau mgeni asijejua siri za jirani. Haisuru, wanaingia katka gumzo, ambapo Mwalimu Majisfu hachoki kumkosoa Mashaka.
Baada ya Dora na Mashaka kujiburudisha kwa chai, iliyosusiwa na Majisifu, kwani siku hizi kakosa tumbo la kuikarisha, sababu yenyewe keshazoea sharabu. Ndipo Mwalimu Majisifu anamwuliza mpwake kazi ambayo angependa kufanya baadaya ya masomo. “Napenda niwe mwandishi wa vitabu kama wewe amu”, (uk 47) akajibu Mashaka. Kwa kumalizia, Majisifu akaboronga lugha, “Kitanda usichokilalia hukijui kunguni wake” (uk 47).
Acha mashaka aulizie muda aliouchukua mwalimu Majisifu kukiandika kitabu chake cha “Kidagaa Kimemwozea”, jawabu likawa kaski mosi. “Aha, kurasa zote hizo?” akaendeleza mashaka. “Mwandishi bora lazima aandike haraka kabla mwazo hayajayeyuka kuwa upepo (uk 48).

Anapoondoka Mashaka, anampasa Mwalimu Majisifu barua inayomwalika Wangwani ili kutoa mihadhara kuhusu uandishi wake. Anamfahamisha Dora ambaye baada ya kuomba kuletewa “rinda na viatu toka Mkokotoni”, anaanza tena kushambuliana. “Kama utaweza, mbwa apige mswaki.” (uk 51). Anaghadhabika Mwalimu na kijibu kwa matusi. Hata hivyo tunajulishwa kwamba “nyoko nyoko” zilikuwa shibe za kawaida kwao.
Amani na Imani wanastakimu pamoja wakiwa na mwano wa kupagazwa, Uhuru. Hapa ndipo tunaelezwa vile wawili hawa walivyokutana na pia yale yaliyowatokea. Nyakti ni za usiku usiku, kuamkia sikukuu ya Uhuru. Wanasokomoko wengine, lao wanalo kushehekea kwa nyimbo na ngoma.
Mwinyihatibu mtembezi ambaye alikuwa mfanyikazi wa Mtemi alinunua shamba kule Baraka, alikoishi na familia yake akina Imani. Basi baba alipofariki, wakaja Askari na kudai kuwa sehemu ile ya ardhi lilikuwa na mwenyewe. Kupinga walipigwa na kuachwa hali mahututi. Oscar Kambona akatorokea na kudai kuja kulipiza kisasi. Baada ya mama mtu kuzikwa, wakaja Askari na kuchoma maskani ile, nusura Imani ateketee.

Marejesho hadi mwanzo wa safari hii ya waja hawa waili. Wanapokutana kando ya ziwa Mawewa, tunapomwona kijana mmoja, umri wa miaka isghirini hivi anaposoma hatujui nini.  Kisha anaitupa runda ile ya makaratasi baharini. Kumbe ilikuwa mswada ambao Amani kapeleka ili kuchapishwa,akarudishiwa kwa madai kwamba haikuwezekana  kuchapishwa. Kumbe Amani kachezewa karata, mswada wake ukaibiwa na kuchapishwa kwa jina la Majisifu Majimarefu. Hapa basi tunashangazwa kuona kwamba ni wale wanaofaa kuwa kiegezo kwa wnagenzi, ndio wanaobadilika kuwa paka kulinda kitoweo.
Wakati ambapo walikuwa wakipiga gumzo usiku kucha, mtoto Uhuru alilala fofofo. Ndugu hawa wa kupanga, wasiojuana, wazaziye Uhuru, mtoto wa kupagazwawakavuliana siri zao. Hata Amani aliyekuwa msiri kama kaburi hakuwa na jingine ila kudondoa alicho nacho rohoni.
Share:

Popular Posts

Unordered List

Pages

Categories

Labels

Download

Powered by Blogger.

Footer Widget 1

Text Widget

Blogger Tricks

Blogger Themes

Categories

Copyright © MWONGOZO NA UCHAMBUZI WA FASIHI ANDISH | Powered by Jkts Company 0706509638 |